Siwezi kwenda mafichoni, nitarudi Tanzania- Lissu - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 30 April 2018

Siwezi kwenda mafichoni, nitarudi Tanzania- Lissu


Mbunge wa Singida Mashariki kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesema kuwa anatarajia kurudi nyumbani Tanzania siku yeyote.
Lissu amekuwa hospitalini akitibiwa tangu septemba 7 mwaka jana aliposhambuliwa nyumbani kwake Jijini Dodoma na watu wasiojulikana.
Amesema kuwa kwasasa amepona na hana tena jeraha lolote wala risasi ndani ya mwili wake, hivyo madaktari waliokuwa wanamtibu ameshamalizana nao.
“Siwezi kwenda mafichoni, siwezi kuikimbia nchi yangu, nitarudi Tanzania, mimi ni mbunge, ni kiongozi bungeni, ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mwanasheria Mkuu wa Chama changu,”amesema Lissu
Hata tangu aanze kupata matibabu amefanyiwa operesheni 17, nne zikiwa sehemu ya tumbo na zingine sehemu mbalimbali za mwili alizokuwa amejeruhiwa

No comments:

Post a Comment