SIMBA KUNUSA UBINGWA LEO - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 16 April 2018

SIMBA KUNUSA UBINGWA LEOSimba inaikaribisha Tanzania Prisons leo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Kikosi hicho kimetoka kupata alama tatu kwenye mechi iliyopita dhidi ya Mbeya City kwa jumla ya mabao matatu kwa moja.

Tayari timu zote zimeshakamilisha maandalizi kuelekea mechi hiyo ambayo itaanza majira ya saa 10 jioni.

Endapo Simba ikishinda mchezo huo itazidi kujiwekea mazingira ya kuzidi kuunusa ubingwa wa ligi kwa kufikisha alama 58 dhidi ya watani zake wa jadi Yanga walio na 47.

No comments:

Post a Comment