SIMBA KUIACHA YANGA KWA ALAMA 14, NI VITA DHIDI YA LIPULI KWENYE LIGI LEO - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 21 April 2018

SIMBA KUIACHA YANGA KWA ALAMA 14, NI VITA DHIDI YA LIPULI KWENYE LIGI LEONa George Mganga

Ligi Kuu Bara inaendelea jioni ya leo kwa mchezo mmoja pekee kupigwa katika Uwanja wa Samora mjini Iringa ambapo wenyeji, Lipuli FC watakuwa wanaikaribisha Simba SC ya jijini Dar es Salaam.

Tayari kila timu imeshamalisha maandalizi yake jana kuelekea mchezo huo ambao utaanza majira ya saa 10 kamili jioni.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Lipuli FC, Clement Sanga, ametamba kuvunja rekodi ya Simba ambayo haijapoteza mchezo wowote katika ligi msimu huu.

Sanga ameeleza wapo tayari kuivunja rekodi hiyo leo, akidai watashinda si chini ya mabao mawili.

Simba wanaivaa Lipuli wakiwa na njaa ya kuukosa ubingwa kwa takribani zaidi ya misimu minne sasa.

Endapo wekundu wa Msimbazi watapata matokeo, watakuwa wanajiweka kwenye mazingira mazuri ya kuutwaa ubingwa kwa kuwaacha watani wao wa jadi kwa alama 14 zaidi.

Simba hivi sasa wamejikusanyia pointi 58 huku Yanga walio na viporo vya mechi mbili wana pointi 47. Kama wakishinda watafikisha pointi 61 huku Yanga wakisalia na hizo 47 kabla ya kucheza viporo vyao.

No comments:

Post a Comment