Shamsa Ford: Tusimlaumu Diamond Kudhalilisha Wanawake, Hawajitambui - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 20 April 2018

Shamsa Ford: Tusimlaumu Diamond Kudhalilisha Wanawake, Hawajitambui

MUIGIZAJI wa Bongo movie, Shamsa Ford amesema si kweli kwamba Diamond anawadhalilisha wanawake anaotoka nao kimapenzi kwa kusambaza video zao mtandaoni.

Diamond amezua gumzo baada ya video yake ya faragha kusambaa mtandaoni akiwa na Hamisa Mobetto na binti wa kizungu.

Kwenye mahojiano na mtandao maalumu, Shamsa aliulizwa nini maoni yake kuhusu jambo hilo akasema Diamond aendelee kutoka na wanawake tofauti kwa kuwa hawajitambui na amemtahadharisha awe makini kwa kuwa kuna magonjwa.

"Mwanaume hawezi kukufanya mwanamke ukawa chombo cha starehe inategemea mwenyewe na akili yako,kama unataka kuchezewa utachezewa kama unataka kuwa mwanamke wa muhimu kwake utakuwa inategemea mwenyewe unajiweka wapi,” amesema Shamsa.

Amesema hawezi kumlaumu Diamond kama anawatumia wanawake maana wenyewe wanapenda kuwa hivyo na kumsihi kuwa makini ili kuepuka magonjwa ya zinaa.

Chanzo: Habari Leo

No comments:

Post a Comment