‘Serikali inawasaidia wajasiriamali’ - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 15 April 2018

‘Serikali inawasaidia wajasiriamali’

WAZIRI wa Biashara na Viwanda, Balozi Amina Salum Ali amesema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inaendelea kuwasaidia wafanyabiashara na wajasiriamali waliopo nchini ili bidhaa wanazozalisha ziweze kuwa viwango bora hali itakayowahakikishia kupata masoko ya uhakika.

Alieleza hayo alipokuwa akizungumza na wajasiriamali wa Zanzibar katika uzinduzi wa klabu za kibiashara, hafla iliyoandaliwa na benki ya NMB, huko katika ukumbi wa Golden Tulip ulioko Malindi mjiniZanzibar.
Alisema serikali inawasaidia wajasiriamalimali hao ili waweze kutimiza malengo yao na waweze kuchangia uchumi wa Zanzibar ambayo malengo yake ni kwamba ifikapo mwaka 2020 iwe imeufikia uchumi wa kati utakaochochewa pia na uwepo wa viwanda.
Alisema klabu za wajasiriamali zinasadia kujenga mawasilino na kuwaunganisha wazalishaji hao na kupata uelewa jinsi ya uendeshaji wa biashara zao.
“Nimeona Pemba walipoelimishwa wakulima wa karafuu benki imeweza kupata wateja wengi, niwapongeze NMB mmefanyakazi nzuri ya kuwaelimisha wananchi umuhimu wa benki na kuweza kupata mitaji kwa ajili ya kujiendeleza”, alisema.
Aidha alisema fursa hiyo ni muhimu sana kwa wajasiriamali na inaonekana benki hiyo inaisadia serikali kwa kuongeza uzalishaji mali na kutoa elimu ya inayoendeleza uzalishaji.
Hivyo aliwataka wajasiria mali hasa wanawake kujiunga na benki hiyo ili kuweza kupata fursa za kibiashara na kuweza kuongeza kipato chao wanapokipata kupitia biashara zao na kukuza biashara.
Nae meneja wa benki hiyo, Badru Iddi, alisema NMB imekuwa ikiwaunganisha wafanyabiashara mbalimbali katika makundi yao ikiwa na lengo la kuwasaidia na kufikia malengo yao ya kibiashara na kujenga uchumi.
NA MADINA ISSA

No comments:

Post a Comment