SERENGETI BOYS KUTUA JUMANNE ALFAJIRI, KUPOKEWA NA WAZIRI MWAKYEMBE - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 30 April 2018

SERENGETI BOYS KUTUA JUMANNE ALFAJIRI, KUPOKEWA NA WAZIRI MWAKYEMBETimu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) iliyokuwa irudi nchini Jumatano Alfajiri sasa inatarajia kurudi Alfajiri ya kuamkia Jumanne Mei Mosi, 2018.

Mabadiliko hayo yametokana na Baraza la Vyama na Vilabu Africa Mashariki na Kati CECAFA kubadili tiketi za ndege za Serengeti Boys.

Serengeti Boys wanaotarajia kutua kwa Shirika la Ndege la Rwanda Alfajiri saa 9 watapokewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe.

Serengeti Boys wametwaa ubingwa huo wa Cecafa baada ya kuifunga Somalia katika mchezo wa fainali iliyochezwa Uwanja wa Ngozi kwa mabao ya EdsonJeremiah na Jaffar Juma Mtoo.

Katika mashindano hayo Serengeti Boys ilitoka sare 1-1 na Uganda kabla ya kuifunga Sudan 6-0 na baadaye kuichapa Kenya kwa mabao 2-1 kwenye nusu fainali na kushinda mabao 2-0 dhidi ya Somalia kwenye mchezo wa fainali

No comments:

Post a Comment