RC.AYOUB "SEKTA YA ELIMU INA CHANGAMOTO NYINGI SANA KATIKA MKOA WANGU UKILIGANISHA NA SEKTA NYENGINE" - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 16 April 2018

RC.AYOUB "SEKTA YA ELIMU INA CHANGAMOTO NYINGI SANA KATIKA MKOA WANGU UKILIGANISHA NA SEKTA NYENGINE"

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud amesema kuwa sekta ya elimu ina changamoto kubwa katika Mkoa huo ulikinganisha na sekta nyengine pamoja na jihida kubwa zinazochukuliwa na serikali katika kuzipatia ufumbuzi. 
Mhe Ayoub ameeleza hayo hapo ofisini kwake vuga wakati akizungumza na uongozi wa Taasisi ya Milele Zanzibar uliofika ofisini kwake kujitambulisha na kuelezea mipango ya utekelezaji wa miradi ya miaka mitatu ijayo.
Amesema kutokana na tafiti za ndani zilizofanya na serikali ya Mkoa imebainika uhaba mkubwa wa madawati na madarasa ya kusomea katika skuli za maeneo mbali mbali ya Mkoa huo mambo ambayo yamekuwa yakipelekea usumbufu kwa walimu na wanafunzi katika upatikanaji wa huduma ya  elimu.
Aidha Mkuu wa Mkoa amesema Serikali ya Mkoa wa Mjini Magharibi ipo tayari kufanya kazi kwa karibu na Taasisi ya Milele Zanzibar katika Sekta za kijamii ikiwemo Afya na Elimu ili kuona wanasogeza kwa karibu huduma hizo muhimu kwa jamii.
Akizungumza Sekta ya Afya Mhe Ayoub amesema kupitia ugatuzi Mkoa umedhamiria kuimarisha sekta hiyo hususani  katika Wilaya za Magharibi ambapo imepanga kuzifanya hospitali ya Mbuzini kuwa hospitali ya Wilaya kwa Magharibi “A”na Hospitali ya Fuoni kwa Wilaya ya Magharibi “B”
Mapema akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa miradi wa taasisi ya Milele Zanzibar  Khadija Abdallah Shariff amesma taasisi yao imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuongeza kasi ya kuwaletea maendeleo wananchi wa visiwa vya Zanzibar katika sekta za elimu,afya na uchumi jamii.
Akielezea mipango ya utekelezaji ya miradi kwa miaka mitatu ijayo amesema pamoja mafanikio makubwa waliyofikia katika utoaji wa huduma mabali mbali kwa jamii kwa sasa taasisi hiyo imekusudia kusaidia katika sekta hizo tatu na kumueleza Mkuu wa Mkoa kuwa wamekusudia kutembele katika miradi ambayo wamesaidia katika Mkoa huo.SAUTI


NA FATUMA MUHAMED

No comments:

Post a Comment