RC,AYOUB MOHAMMED AWATAKA WANANCHI WAKE KUCHUKUA TAHADHARI KATIKA KIPINDI HICHI CHA MVUA ZA MASIKA - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 15 April 2018

RC,AYOUB MOHAMMED AWATAKA WANANCHI WAKE KUCHUKUA TAHADHARI KATIKA KIPINDI HICHI CHA MVUA ZA MASIKA

Related image
Mkuu wa Mkoa Mjiniagharibi Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud  amewataka wananchi wa Mkoa huo kuchukua tahadhari maalum katika kipindi hiki cha masika kuhama maeneo hatarishi ili kunusuru maisha yao na mali zao.
Akitoa Taarifa maalum kwa wananchi wa Mkoa huo kupitia Kituo cha Television ya ZBC TV huko Mnazi mmoja amesa ni vyema wananchi kuhama kwenye maeneo ya njia za maji na mabonde.
Amesema taarifa za wataalam wa hali ya hewa zinaeleza kuwa mvua itakuwa kubwa kipindi cha siku 5 kuanzia jana hadi jumaane ijayo,hivyo amewasihi kufitilia kwa karibu taarifa za hali ya hewa ili kujihadhari zaidi.
Aidha ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao kipindi cha kuwapeleka skulo na chuoni wasicheze katika misingi ma maeneo yanayotua maji.
Hata hivyo Mhe Ayoub amewatahadharisha wananchi wanatumia njia Mwanakwerekwe na Fuoni kutumia barabara mbadala kwani maeneo hayo yameshajaa maji na kufunika njia hizo.
Mhe Ayoub amesema katika mvua hii ya siku 2 zaidi ya nyumba mia moja zimeingia maji na kusanabisha hasara kwa familia na wakaazi wa nyumba hizo katika Shehia ya Sebleni Wilaya ya Mjini Unguja.

No comments:

Post a Comment