RC.AYOUB MOHAMED MAHAMUOD AMESEMA JUMLA YA NYUMBA ELFU MOJA 552 ZIMEATHIRIKA NA MVUA - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 17 April 2018

RC.AYOUB MOHAMED MAHAMUOD AMESEMA JUMLA YA NYUMBA ELFU MOJA 552 ZIMEATHIRIKA NA MVUA

MKUU WA MKOA WA MJINI MH AYOUB MOHAMED MAHAMUOD AMESEMA JUMLA YA NYUMBA  ELFU MOJA  552 ZIMEATHIRIKA NA MVUA ZA MASIKA ZINAONDELEA KUNYESHA AMBAZO ZIMEAMBATANA NA UPEPO MKALI  KATIKA MKOA WA MJINI MAGHARIBI  KWA KIPINDI CHA SIKU NNE. 
AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI HUKO OFISINI KWAKE VUGA AMESEMA HATUA HIYO   IMEWAFANYA WATU ZAIDI YA WATU ELFU KUMI KUKOSA MAKAZI  PAMOJA NA MIUNDOMBINU KUHARIBIKA KUTOKANA NA ATHARI ZILIZOTOKANA NA MVUA HIZO.
MH AYUOUB AMEFAFANUA KATI YA NYUMBA HIZO 16 ZIMEANGUKA KUTA NA , ELFU MOJA NA 90 ZIMEINGIA MAJI NA KUSABABISHA WANANCHI KUHAMA  KATIKA  MAJUMBA  YAO  NA  HUKU  NYUMBA   MIA NNE NA 46 ZIMEINGIA MAJI NA WAKAAZI   HAO   BADO WAMEBAKIA NDANI YA NYUMBA ZAO.


HATA HIVYO AMESEMA HALI HIYO BADO HAIJAFIKIA KIWANGO KIKUBWA UKILINGANISHA MIAKA ILIYOPITA YA 2015-2017 HIVYO NI VYEMA WANANCHI WAKACHUKUA TAHADHARI  ZA KUJIKINGA ILI HALI HIYO ISIJIREJEE .
AKIZUNGUMZIA SUALA LA USAFI KATIKA MKOA WAKE AMESEMA JUMLA YA MAGENGE12   YAMEFUNGIWA   KATIK  MKOA  WA  MJINI  MAGHARIBI   KUTOKANA   NA KUKIUKA TARATIBU ZA USAFI AMBAZO   ZINAHATARISHA   AFYA   ZA   WANANCHI.


PIA AMEWATAKA WAFANYABIASHARA KUFUATA TARATIBU ZA KIAFYA KWA KUZINGATIA AFYA  ZA  WANANCHI KWANI SERIKALI IMEKUWA MSTARI WA MBELE KUHAKIKISHA WANANCHI WAKE HAWAPATI MARADHI  YANAYOTOKANA NA UCHAFU.
AIDHA AMEWATAKA MADEREVA WA GARI ZA ABIRIA KUACHA MARA MOJA TABIA YA KUZIDISHA  NAULI  KUWA KUBWA   KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA  AMBAYO IKO KINYUME NA NAULI LIYOPANGWA NA SERIKALI KWANI KUFANYA HIVYO KOSA KISHERIA NA KWAMBA WATACHUKULIA HATUA WATAKAOKWENDA KINYUME NA UTARATIBU HUO.
FATMA MOHD

Na Fatuma Mohamed


No comments:

Post a Comment