RC.AYOUB AWAAGIZA MAOFISA WA ELIMU KUKUTANA KWENYE VIKAO KILA MWEZI ILI KUJUA CHANGA MOTO - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 15 April 2018

RC.AYOUB AWAAGIZA MAOFISA WA ELIMU KUKUTANA KWENYE VIKAO KILA MWEZI ILI KUJUA CHANGA MOTO

Image result for ayoub mohamed mahmoud
MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud amewaagiza maafisa wa Elimu wa Wilaya na Mkoa huo kukutana na bodi ya elimu ya Mkoa kila baada ya mwenzi mmoja badala ya mienzi mitatu ili kuona wanazikabili changamoto za sekta ya elimu katika Mkoa huo.

 Mhe A youb amesema hayo alipokuwa akizungumza na maaofisa Wilaya ya Mkoa, Mwenyeviti wa Skuli za Mkoa pamoja na walimu wakuu katika kutathmini elimu katika Mkoa kikao ambacho kimefanyika kwenye  ukumbi wa Skuli ya Haile Selassie.
Amesema kukutana na bodi elimu ya Mkoa  kutarahisisha kujua changamoto zinazokabili sekta ya elimu katika skuli mbali mbali za Mkoa huo sambamba na kutathmini masuala yanayowakabili kuzipatia ufumbuzi  kwa wakati na muda anaofaa.
Aidha Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa elimu kimkoa haipo vizuri sana kwani matokeo ya mitihani kitaifa ya kila mwaka yanayojitokeza katika Mkoa huo ambapo mwaka 2016 matokeo ya kidato cha sita ilionesha kuwa skuli saba za mwisho katika skuli 10 za Tanzania zilikuwa ni za Mkoa huo ambapo mwaka 2017 kwa matokeo ya kidato cha nne yameonesha kuwa Skuli mbili za Mkoa huo ambazo zimo katika Skuli kumi za mwisho kwa Tanzania nzima na kimkoa imekuwa ni wa 25 katika Mkoa 31 ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisema katika matokeo hayo hakuna anayefurahia kwani watoto wamekuwa wanashindwa kupata matokeo mazuri na kushindwa kuendelea mbele zaidi kimasomo,Hivyo  amewasisitiza Walimu na wazazi kushirikiana kwa pamoja ili kuona matokeo mabaya katika skuli za Mkoa huo yanaondolewa mara moja.
Akizungumzia suala la udhalilishaji Ayoub alisema ataendelea na kusimamia sheria bila ya kumuonea mtu ama kumuogopa hivyo atakayebainika kufanya vitendo vya udhalilishaji atahakikisha atasimamia na hatorudi nyuma na kuhakikisha sheria inachukua nafasi yake ili kuona vitendo hivyo vinamalizika
Nao walimu wakuu wan a Wenyeviti wa kamati za skuli za mkoa wa mjini na wamesema wakati umefika wa kukabilia na vitendo vinavyopeleka uvunjifu wa sheria kwa kutomuonea muhali mtu atakayebainika kufanya vitendo hivyo.
Aidha walisema wameiomba serikali kupitia wizara ya elimu kuangalia tena mitaala ya elimu ili kuona sekta hiyo inaendelea kuimarika sambamba na kuahidi kukaa pamoja kuhakikisha changamoto zilizopo zinaondoka ili maendeleo ya wanafunzi yanakuwa  mazuri.

NA MZEE GEORGE.

No comments:

Post a Comment