Polisi Kumuhoji Tena Daimond Sakata la Kuvujisha Video - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 18 April 2018

Polisi Kumuhoji Tena Daimond Sakata la Kuvujisha Video

Baada ya hapo jana April 16, 2018 msanii Diamond kuhojiwa na Polisi kufuatia kusambaza video zisizo na maadili mtandaoni, msanii huyo anatarajiwa kuhojiwa tena.Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kushikiliwa kwa Diamond hapo jana kwa ajili ya mahojiano ila sasa ameachiwa kwa dhamana wakati uchunguzi zaidi unaendelea na utakapokamilika ataitwa tena polisi kwa mahojiano.Taarifa za kuhojiwa Diamond na Polisi simesikika kwa mara ya kwanza leo Bungeni ambapo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe alisema Polisi walimkamata Diamond hapo jana, pia aliangiza msanii Nandy nae ahojiwe.Hapo Juzi April 15, 2018 Diamond aliweka video mbili mtandaoni zisizo na maadili akiwa na wanawake wawili tofauti. Kabla ya hilo ilivuja video mtandaoni ikimuonyesha msanii Nandy akiwa faragha na msanii mwenzie, Bill Nass.

No comments:

Post a Comment