Picha/Video: Barcelona walivyosherehekea kushinda ubingwa La Liga msimu huu - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 30 April 2018

Picha/Video: Barcelona walivyosherehekea kushinda ubingwa La Liga msimu huu

Raha ya soka ni kushinda ubingwa. Usiku wa jana Barcelona walifanikiwa kushinda kombe la ligi kuu ya Hispania (La Liga) baada ya kuifunga Deportivo kwa mabao 4-2 ikiwa zimebakia mechi chache kumalizika kwa ligi hiyo.
Mabao ya Barca yalifungwa na Philippe Coutinho dakika ya sita na Lionel Messi aliyefunga hat trick (6,81 na 86). Nao Deportivo walipata mabao yao kupitia kwa Perez (39) na Colak (63).
Video Player
00:00
00:06
Kutokana na kushinda taji hilo Barca wanakuwa wameshinda ubingwa wa La Liga mara saba ndani ya misimu 10. Furaha ya wachezaji wa Barcelona ilikuwa kubwa mpaka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ikiwa ni kombe lao la pili kushinda kwa msimu huu.

Mashabiki wa Barcelona wakishangilia mitaaniNo comments:

Post a Comment