Picha: Wanajeshi JWTZ watunukiwa Nishani za UN - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 18 April 2018

Picha: Wanajeshi JWTZ watunukiwa Nishani za UN

Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kikosi cha 11 wametakiwa kujivunia mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha mwaka mmoja waliokuwa wakishiriki Ulinzi wa amani Jimboni Darfur nchini Sudan na kutunukiwa Nishani za Umoja wa Mataifa (UN).


Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa UNAMID jimboni Darfur, Luteni Jenerali Leonard Ngondi wakati wa sherehe za kuwatunuku Nishani Askari wa JWTZ katika sherehe zilizofanyika Khor Abeche.
“Kutunukiwa nishani ni jambo la Kujivunia kwa kuwa zimetolewa kwa sababu Askari wamefanya kazi Nzuri ambayo inapaswa kupongezwa hasa kutokana na Doria zilizofanyika ikiwemo katika safu za Milima ya jaber ambayo inakaliwa na waasi” alisema Luteni Jenerali Ngondi.


Kwa Upande wake Mkuu wa Operesheni ya Jaber Mara Lameck Kawiche alitoa wito kwa Wanajeshi wa Tanzania kuendeleza utayari wao ili kuhakikisha wanalinda heshima ya jeshi hilo kwa kufanya kazi kwa Weledi ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea kama ilivyotokea Nchini Kongo.

No comments:

Post a Comment