Picha: Ndoa ya Alikiba yaelekea kuwa moto, watu wa karibu waanza kutua Mombasa - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 18 April 2018

Picha: Ndoa ya Alikiba yaelekea kuwa moto, watu wa karibu waanza kutua Mombasa

Ujio wa ndoa ya Alikiba kwa sasa ndio imeteka vichwa vya habari mjini.
Tayari maandalizi muhimu yameonekana kuanza kukamilika huku watu wa karibu wa msanii huyo wameonekana kuanza kutua mjini Mombasa, Kenya kwa ajili ya kuhudhuria ndoa hiyo.
Baadhi ya picha tayari zimeanza kusambaa mitandaoni zikiwaonyesha watu hao akiwemo msanii wa filamu Bongo, Esha Buheti na dada yake Alikiba, Zabibu na wengine.
Wakati huo huo Abdu Kiba ameweka moja ya picha hizo kwenye mtandao wa Instagram na kuandika ujumbe unaosomeka, “MY TEAMMombasa kitaelewekaa tu.”
Alikiba anatarajiwa kufunga ndoa na mrembo Aminah Rikesh April 26, 2018 katika ukumbi wa Diamond Jubilee uliopo mjini Mombasa.

No comments:

Post a Comment