Mkuu wa zamani wa FBI Asema Trump Hana 'Maadili ya Uongozi - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 16 April 2018

Mkuu wa zamani wa FBI Asema Trump Hana 'Maadili ya Uongozi

Mkuu wa zamani wa FBI  Asema Trump Hana 'Maadili ya Uongozi
Aliyekuwa mkuu wa shirika la upelelezi Marekani FBI James Comey amesema Donald Trump 'hana maadili ya uongozi kushikilia wadhifa wa rais' na ambaye anawachukulia wanawake kama 'kiteweo cha nyama'.

Bwana Comey alikuwa akihojiwa kwa mara ya kwanza kwenye televisheni tangu afutwe kazi na rais Trump mwaka jana.

Ameliambia shirika la habari la ABC kwamba Trump huzusha urongo kila saa na huenda amezuia haki itetendeke.

Saa chache kabla ya mahojiano hayo yapeperushwe, rais Trump alimshambulia Bwana Comey kwa kile anasema ni kusema 'urongo mwingi'.

Comey amekiambia kipindi cha ABC Jumapili usiku: 'Siamini madai yaliopo kumhusu kwamba ana matatizo ya kiakili au katika hatua za kwanza kuugua ugonjwa wa kusahau.'

'Sidhani kwamba ana mapungufu ya kiafya kumuwezesha kuwa rais. Nadhani hana maadili ya kuwa rais'.

"Rais wetu ni lazima aheshimu na afuate maadili ambayo ndio mzizi wa nchi hii. La muhimu zaidi ikiwa ni ukweli. Rais huyu hana uwezo wa kufanya hivyo," Comey amesema.

Baada ya mahojiano kupeperushwa, chama cha Trump - kupitia kamati ya kitaifa ya Republican - kilitoa taarifa ikisema kuwa hatua ya Comey kujitokeza mbele ya umma kunadi kitabu chake imeonyesha kwamba, "utiifu wake wa juu ni kwake mwenyewe".

Trump amuonya mkuu wa FBI aliyefutwa James Comey
Rais Trump achukizwa na tuhuma za Comey
Trump atetea hatua ya kumfuta Comey
"Kitu kibaya zaidi kushinda historia ya ukosefu wa nidhamu wa Comey ni kukubali kwake kusema chochote ili aweze kuuza vitabu," taarifa hiyo ilisema.

Je tumefikaje hapa?
Hadithi hii inaanzia wakati wa uchaguzi wa urais mnamo 2016, wakati Bwana Comey alikuwa mkurugenzi wa FBI director, na uchunguzi kuhusu namna mgombea wa urais wa chama cha Democrat Hillary Clinton alivyozishughulikia barua pepe za siri katika kompyuta binafsi wakati akiwa waziri wa mambo ya nje.

Mnamo Julai 2016, Comey alisema kwamba hakuwa na umakini katika namna alivyozishughulikia barua pepe hizo, lakini FBI haitomshtaki.

Hatahivyo mnamo Oktoba, sikukadhaa kabla ya uchaguzi, alituma barua bungeni akiliarifu kwamba FBI linaanzisha upya uchunguzi baada ya kugundua barua pepe zaidi.

Barua hiyo ilifichuliwa kwa umma - na Hillary Clinton akasema hatua hiyo ndiyo iliompa Trump ushindi.

Mnamo November, FBI lilisema limekamilisha ukaguzi wa barua pepe hizo mpya zilizogunduliwa na kwa mara nyingine likasema halitomshtaki.

Na bwana Trump alipopata urais, Bwana Comey alisema kuwa alijaribu kumshurutisha aape kumtii - Jambo ambalo rais analikana pakubwa.

Mnamo Machi 2017, wakati uchunguzi ulipokuwa unafanywa na FBI kuhusu tuhuma za ushirikiano kati ya timu ya kampeni ya Trump na Urusi inatuhumiwa kwamba Trump alimshinikiza Comey kutangaza wazi kwamba rais hatochunguzwa kibinafsi - jambo ambalo mkurugenzi huyo wa zamani wa FBI alikataa kufanya hivyo.

Baadhi ya wanasiasa wa Democrats walimlaumu Comey kwa kumfanya Bi Clinton apoteze kura katika uchaguzi , huku wafuasi wa Trump walihisi kwamba anamlenga rais katika uchunguzi huo.

Alifutwa kazi na rais Trump mwezi Mei, na alipata taarifa kuhusu kutimuliwa kwake katika vyombo vya habari nchini.

Comey alihojiwa bungeni kuhusu uchunguzi huo wa uwezekano kuwepo uhusiano kati ya kampeni ya Trump na Urusi na kutimuliwa kwake, na alimthumu rais kwa kusema urongo na kumchafulia jina. 

No comments:

Post a Comment