Mke wa Rommy Jones Afunguka Mazito Mumewe Kumtongoza Naj - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 16 April 2018

Mke wa Rommy Jones Afunguka Mazito Mumewe Kumtongoza Naj

Mke wa Rommy Jones Afunguka Mazito Mumewe Kumtongoza Naj
WIKIENDI iliyopita, mume wa mtu, Romeo Jones ‘Rommy’ ambaye ni kaka na DJ wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alichafuka kufuatia meseji zake akimtongoza msanii wa Bongo Fleva, Najma Dattan ‘Naj’ kuvuja ambapo ilisemekana kuwa, mkewe Kahuye Jord almaarufu Kay Jord alimaindi na kusababisha ndoa yao kutikisika.


Kwenye meseji hizo, Rommy anamtaka kimapenzi Naj ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Baraka Andrew ‘Barakah The Prince’ ambapo zilionesha akimponda na kudai Barakah anamshusha nyota yake.

Kufuatia skendo hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta mke wa Rommy na kumuuliza analichukuliaje suala hilo ambapo alifunguka kwa mara ya kwanza tangu kuzagaa kwa tuhuma hizo nzito dhidi ya mumewe.

Kay Jord alifunguka kuwa, kwenye meseji hizo zilizodaiwa kwamba mumewe alikuwa akimtongoza Najma, haziendani na ukweli kwani asilimia kubwa zilionekana ulikuwa ni utani.

“Nimesikia na watu wamesema mengi kuwa mimi nimeondoka nyumbani, kisa hizo meseji, jambo ambalo siyo kweli kabisa.

“Hakuna ukweli kwenye jambo hilo ndiyo maana niliamua kukaa kimya,” alisema mke huyo wa Rommy.

Mwanamama huyo alisema kuwa, yuko vizuri kwenye ndoa yake kama kawaida na hakuna ambacho kimetetereka.Kwa upande wake, Rommy alilieleza Ijumaa Wikienda kuwa, yeye ni mfanyabiashara na Najma wanafahamiana vizuri.

Alisema kuwa, kuhusiana na hizo meseji anazodai kumtongoza Naj ilikuwa ni utani wa kawaida tu.

Rommy na Barakah waliingia kwenye mgogoro mzito baada ya Barakah kuonesha meseji hizo kwenye mitandao ya kijamii huku akimtukana na kudai kuwa, Rommy alikuwa akimtongoza mpenzi wake huyo. 

No comments:

Post a Comment