Meneja wa Kitengo cha Hahari (MPRU) Atumbuliwa Kisa Hiki Hapa - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 16 April 2018

Meneja wa Kitengo cha Hahari (MPRU) Atumbuliwa Kisa Hiki Hapa

Meneja wa Kitengo cha Hahari (MPRU) Atumbuliwa Kisa Hiki Hapa
Waziri wa  Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amemsimamisha kazi Meneja wa kitengo cha bahari na maeneo tengefu (MPRU) Dr Milali Machumu kwa kushindwa kusimamia ipasavyo kitengo hicho. Pamoja na kusimamishwa Mpina ameagiza achunguzwe. Maamuzi hayo yamekuja kufuatia taarifa ya ukaguzi wa ufanisi katika usimamizi wa hifadhi za bahari na maeneo tengefu kubainisha madhaifu.

Waziri Mpina amesema…>>>“Kwa mamlaka niliyonayo kulingana na sheria ya kitengo cha hifadhi za bahari na maeneo tengefu, Namba 29 ya mwaka 1994 nanatoa maelekezo yafuatayo”

Namsimamisha kazi Meneja wa kitengo cha bahari na maeneo tengefu (MPRU) Dr Milali Machumu mara moja kwa kushindwa kusimamia ipasavyo kitengo hiki, pamoja na kumsimamisha kazi pia atachunguzwa
Ninavunja Bodi ya wadhamimi mara moja na kuisuka upya
Ninamwagiza Katibu mkuu wa Uvuvi katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuunda kamati ya uchunguzi kuhusu utendaji kazi wa Meneja 

No comments:

Post a Comment