Mchopanga: Nina siri Nzito ya Masogange Nitausema Siku ya Mazishi - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 21 April 2018

Mchopanga: Nina siri Nzito ya Masogange Nitausema Siku ya Mazishi

Mchopanga: Nina siri Nzito ya Masogange Nitausema Siku ya Mazishi
Msanii wa filamu Juma Chikoka maarufu kama 'Chopa wa Mchopanga' anayedai ameshuhudia dakika za mwisho za kupigania uhai wake msanii wa muziki ‘Video Queen’, Agnes Gerald, maarufu Masogange' amesema mrembo huyo amemuachia ujumbe mzito ambao atausema siku ya mazishi.

Chopa ameyasema hayo jana wakati wa kikao cha dharura cha wasanii kuhusu maandalizi ya mazishi yake yanayotarajiwa kufanyika Jumatatu Jijini Mbeya ingawa ataagwa kwenye viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam kesho.

Msanii huyo ambaye ni mmoja wa marafiki wa karibu  wa Masogange, amesema dakika chache kabla hajafariki alikuwa kalala mapajani kwake na walizungumza vitu vingi ikiwemo kumpa ujumbe wa kuwaeleza Watanzania.

“Tuliongea mengi lakini kuna makubwa mawili ambayo aliniagiza niwaambie Watanzania, ila hilo nitalifanya kwa kuongea na vyombo vya habari na kuona namna sahihi ya kusaidiana kama vijana, hatupaswi kuingizana katika matatizo.

“Kwa sasa siwezi kusema alichoniambia, embu ngoja tumalize shughuli ya kumhifadhi halafu nitayaweka wazi aliyoniambia, kwani kwa sasa haitaleta picha nzuri na watu wanaweza kutafsiri ndivyo sivyo,”amesema.

Chopa amesoma alikuwa akimtembelea Masogange, tangu alazwe katika Hospitali ya Mama Ngoma. Amesema alilazwa hospitali kwa siku nne.

“Ugonjwa uliokuwa unamsumbua mbali na pumu, pia kupungukiwa damu, jana (juzi) nilikuwa nimejipanga kwa ajili ya kumtolea damu lakini ndio hivyo hakuweza kumaliza siku,” amesema.

Msanii huyo anasema amefahamiana na Masogange wakati akiwa Agnes Gerald na si Masogange, urafiki ambao umedumu hadi mauti yanamfika. 

No comments:

Post a Comment