Manara aibuka kwa mara ya kwanza baada ya kuifunga Yanga ‘subirini tunyanyue ndoo ndio mtajua nafananaje’ - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 30 April 2018

Manara aibuka kwa mara ya kwanza baada ya kuifunga Yanga ‘subirini tunyanyue ndoo ndio mtajua nafananaje’

Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara ameibuka kwa mara ya kwanza na kuzungumza tangu timu yake ifanikiwe kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1 – 0 mbele ya mtani wake wa jadi Yanga SC kwenye mchezo wa ligi kuu uliyopigwa hapo jana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Manara amesema kuwa mashabiki wa klabu hiyo wanamfanya kuwa mfalme siku zote huku akiahidi kuonyesha namna furaha yake ilivyo pale watakapo fanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu wa 2017/18.
Thanks our fans..mnanifanya niwe mfalme always..hii ni trela subirini tunyanyue ndoo ndio mtajua nafananaje…rafiki yangu kinje Ngombale kaniambia sijaja mpirani miaka mingi ila ww umenirudisha..hahahahaha yes mm ndio spokesman namba one wa taifa hili
Simba imwfanikiwa kuchomoza na pointi tatu kwenye mchezo huo uliyo wakutanisha watani wao Yanga baada ya kupata bao moja na la pekee kutoka kwa beki wake, Erasto Nyoni lililofungwa dakika ya 37 kipindi chwa kwanza.

No comments:

Post a Comment