MAKONDA AMPOKEA AHMED ALIYEPOOZA AKITOKEA CHINA - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 30 April 2018

MAKONDA AMPOKEA AHMED ALIYEPOOZA AKITOKEA CHINA

Makonda akisalimiana na ndugu zake Ahmed Albaiti katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  leo Jumatatu, Aprili 30, 2018 amempokea kijana, Ahmed Albaiti aliyekuwa nchini China kwa ajili ya matibabu kutokana na kupooza mwili wake.
Albaiti aliyepelekwa na Makonda huko China baada ya tatizo hilo lililomsababishia kukaa kitandani kwa miaka 10, amerejea leo na kulakiwa na wananchi waliojitokeza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Akizungumza wakati wa mapokezi hayo, Makonda amewashukuru Watanzania waliowezesha kupatikana kiasi cha fedha ambazo zimetumika katika matibabu ya kijana huyo.
Ahmed alikwenda nchini China miezi miwili iliyopita ambapo hali yake inaendelea vizuri  baada ya kupatiwa matibabu.
Kijana huyo alipata tatizo hilo la kupooza baada ya kuumia wakati akifanya mazoezi ya kuogelea.
Ahmed Albaiti akiwasili uwanja wa ndege Dar es Salaam akitoka katika matibabu nchini China leo.

No comments:

Post a Comment