Lwandamina Awapa Matumaini Yanga Aungana na Timu Hiyo Ethiopia - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 18 April 2018

Lwandamina Awapa Matumaini Yanga Aungana na Timu Hiyo Ethiopia

Lwandamina Awapa Matumaini Yanga Aungana na Timu Hiyo Ethiopia
Aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, George Lwandamina ameungana na timu yake hiyo ya zamani kwa kuandika ujumbe unaoitaka kuhakikisha inachomoza na ushindi dhidi ya wapinzani wao Welayta Dicha kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika unaotarajiwa kupigwa hii leo majira ya saa 10:00 alasiri.


Katika kuonyesha mapenzi yake kwa wanajangwani hao na bado yupo pamoja nao, Lwandamina ameamua kuungana na Yanga SC kwenye kipindi hiki kwa kuandika ujumbe huo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Facebook.

Ushindi ni fikra inayofurahisha nafsi ya kila kitu. Kila lakheri vijana.

Lwandamina ameandika maneno hayo ambayo yatakayo leta faraja kwa mashabiki na wachezaji wa Yanga SC na hamasa wakati wakiwa wanakabiliwa na mechi dhidi ya Welayta Dicha michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika. 

No comments:

Post a Comment