Lulu atoa zawadi kwa watoto Muhimbili kwenye birthday yake - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 16 April 2018

Lulu atoa zawadi kwa watoto Muhimbili kwenye birthday yake

April 16 kama ya leo miaka kadhaa iliyopita alizaliwa Elizabeth ‘Lulu’ Michael ambaye kwa sasa yupo gerezani akitumikia kifungo cha miaka miwili.
Katika kusherehekea siku hii, mrembo huyo ameamua kutoa zawadi kwa watoto ambao wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Muhimbili.
Zawadi hizo ziliwakilishwa na mama yake mzazi pamoja na msanii mwenzake wa karibu zaidi Dokta Cheni. Lulu pia ametoa ujumbe wa kuwafariji wagonjwa hao pamaoja na wazazi wao.
Ujumbe huo ambao ulisomwa kwa niaba na Dokta Cheni umesema, “Nawapenda sana watoto na nawaombea kwa Mungu. Naamini wakiwa huru kumuomba Mungu na wao wazazi hayo maradhi yanayowakabili yatapona kwa muda mfupi. Ninawatakia kila la kheri na muweze kupona haraka.”

No comments:

Post a Comment