Kocha wa Mwenge FC awatupia lawama waamuzi kwa kuchezea kichapo - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 18 April 2018

Kocha wa Mwenge FC awatupia lawama waamuzi kwa kuchezea kichapo

Related image
BAADA ya Klabu ya Mwenge FC kupokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Jamhuri  Kocha Msaidizi wa timu hiyo Zuber  Haji Zuber amewatupia lawama Waamuzi wa mchezo huo akidai kuwa wamechezesha ovyo.
Mwenge ilikubali kichapo hicho katika mfululizo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Pemba, uliopigwa uwanja wa Gombani Visiwani hapa.
Akizungumza na Mwanaspoti mara baada ya kumalizika kwa pambano hilo Kocha huyo alisema Waamuzi wa mchezo huo hawakuchezesha kwa misingi ya uadilifu .
Alisema katika mchezo huo Muamuzi wa kati hakuchezesha kwa misingi ya uadilifu na kuzikiauka sheria 17 za soka.
Zuber alisem Muamuzi  huyo alikuwa akiangalia upande wa timu pinzani huku faulu na panalt za wazi hakuzitoa jambo ambalo lilisababisha kupoteza mchezo huo.
Hata hivyo alisema kuwa wachezaji wake wakifanyiwa madhambi alikuwa mwepesi kuyaona  na kuzifanyia kazi  lakini upande mwngine hakufanya hivyo.
“Ukweli kwamba imeonekana dhahiri sisi ametuonea kwa kuisadia Jamhuri ishinde mambo tunayofanyiwa kuumizwa wachezaji wetu hakuna kadi hata moja iliyotolewa “alisema.
“Kipa wetu namba moja  aliumizwa  na wapinzani wetu na kulazimika kubakia nje lakini cha kuskitisha hata kadi ya Onyo njano hakumpa”alisema.
Alisema mbali ya kupoteza kwa mchezo hakuna timu itayofika waondoa kwenye kiti cha Uongozi kutoka na pointi nyingi walizonazo katika msimamo wa ligi kikubwa walitaka kulinda heshma ya timu yao.
Mwenge inashika nafasi ya kwanza baada ya kujikusanyia alama 50 huku wapinzani wao wakishika nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 44 na kuishusha Opec hadi nafsi ya tatu iliyokuwa inashika nafasi hiyo ikiwa na alama 43 .
NA SALMIN J.SALMIN

No comments:

Post a Comment