KIIZA AIPA SIMBA ASILIMIA 80 YA UBINGWA, LAKINI - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 17 April 2018

KIIZA AIPA SIMBA ASILIMIA 80 YA UBINGWA, LAKINIMshambuliaji wa zamani katika klabu za Yanga na Simba, Hamis Kiiza, ametoa maoni yake kuelekea ubingwa wa ligi kuu bara msimu huu akiipa Simba asilimia 80 ya kubeba kikombe.

Kiiza ameeleza kuwa Simba wapo vizuri msimu huu kuliko Yanga ambayo haiko kwenye wakati mzuri haswa kiuchumi lakini akisema bado kila timu ina nafasi.

Mchezaji huyo ambaye maisha yake ya soka hivi sasa yamehamia Ethiopia, amesema bado kila timu ina nafasi hivyo ameipa Simba hizo asilimia 80 kutokana na ubora wa vikosi vya timu mbili.

Simba ipo kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 58 huku Yanga ikiwa ina pointi 47 lakini ikiwa nyuma kwa michezo miwili.

Watani hao wa jadi wanatarajia kukutana katika mechi ya mzunguko wa pili Aprili 29 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


CHANZO: E SPORTS - EFM

No comments:

Post a Comment