Kesi ya Abdul Nondo yaahirishwa Mahakama ya Iringa - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 18 April 2018

Kesi ya Abdul Nondo yaahirishwa Mahakama ya Iringa

Kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa, imeahirishwa leo (Jumatano).
Kesi hiyo imeahirishwa kutokana na hakimu kuwa na kesi nyingi na hivyo kuomba kupumzika.
Wakati huo huo upande wa Jamhuri ulifika na mashahidi wanne kati ya watano wanaotakiwa kutoa ushahidi huku mmoja akishindwa kufika mahakamani hapo.
Nondo anashtakiwa kwa makosa mawili ikiwemo kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni March 7 ya mwaka huu kuwa maisha yake yapo hatarini akiwa katika eneo la Ubungo na kuzisambaza kwenye mtandao wa Whatsapp.
Kosa la pili limetajwa kuwa ni kutoa taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma Mafinga wakati alipokuwa akitoa taarifa katika kituo cha polisi mjini humo kwa kusema kuwa alitekwa na watu wasiojulikana.

No comments:

Post a Comment