KATIBU TAWALA WILAYA YA WETE AWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI JUU YA MARADHI YA MRIPUKO - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 21 April 2018

KATIBU TAWALA WILAYA YA WETE AWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI JUU YA MARADHI YA MRIPUKO

katibu tawala wilaya ya wete mkufu faki ali amewataka wananchi wa
wilaya  hiyo kuchukua tahadhari kwa kuweka mazingira  safi  na
kujikinga na maradhi ya miripuko .

kauli hiyo ameitowa wakati  akizungumza na wajumbe wa kamati ya maafa
ya wilaya hapo ofisini kwake wete mkoa wa kaskazini pemba.

amesema kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha  ni vyema  wananchi
kuchukuwa tahadhari za maksudi kusafisha maeneo yao pamoja  na kuondoa
 miti hatarishi  iliokaribu na makaazi  ambayo inaweza kusababisha
maafa.

aidha amesema kumekuwa na baadhi ya wananchi hujenga kwa maksudi
katika maeneo  hatarishi kwa lengo la kuona kwamba serekali  itatoa
misaada kwa waathirika wa maafa hayo.

wakichangia katika kikao hicho wajumbe wa kamati  hiyo ya maafa
wamesema ni vyema kutolewa elimu kwa wananchi juu ya uwekaji wa
mazingira  safi katika kipindi hichi cha mvua  ikiwemo kuchemcha maji
kabla ya kunywa  kuweka dawa za water gurd kusafisha mitaro ya maji
machafu pamoja na kunawa kwa  sabuni  wanapotoka  chooni.

No comments:

Post a Comment