Jaji Mkuu ziarani Pemba leo - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 17 April 2018

Jaji Mkuu ziarani Pemba leo


JAJI Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, amewasili kisiwani Pemba kwa ziara ya siku nne, ambapo akiwa kisiwani humo, atatembelea mahakama, vyuo vya mafunzo na kuzungumza na watendaji wake.
Kwa mujibu wa ratiba iliotolewa na mtandao wa pembatoday kuipata, inaeleza kuwa, ziara hiyo ataanzia Chuo cha Mafunzo Tungamaa wilaya ya Wete, ambapo hapo atawasili majira ya saa 3:00 na kuondoka majira ya saa 5:00 asubuhi.
Aidha leo hii pia, akitoka hapo Jaji huyo Mkuu na ujumbe wake, atakwenda Chuo cha Mafunzo Wete, ambapo akiwa hapo atazungumza na wanafunzi wa chuo cha mafunzo na Maofisa wa vyuo, na kisha kihitimisha ziara yake kwa leo hii April 17.
Kesho April 18, Jaji Mkuu wa Zanzibar ataanza ziara yake majira ya saa 2:30 hadi 4:00  Mahakama ya Mwanzo Micheweni, na kisha kuzungumza na wafanyakazi, kisha kwenda Konde kuzungumza na watendaji wa Mahakama wilaya, kabla ya kwenda Wete majira ya saa 5:30 hadi saa 6:30 na kuitembelea na kuzungumza na wafanyakazi wa Mahakama ya Ardhi Wete.
April 19 Jaji Mkuu wa Zanzibar atakuwa mjini Chakechake kwa kuanza ziara yake, kuitembelea Mahakama ya Mwanzo, kisha saa 4:00 hadi saa 5:00 asubuhi akiitembelea Mahakama ya Ardhi iliopo Machomane, ambapo siku hiyo hiyo atatembelea Mahakama ya Mwanzo Kengeja na kumalizia ziara yake Mahakama ya wilaya Mkoani.
Ijumaa ya April 20, Jaji Mkuu ataitembelea Mahakama kuu Chakechake na kisha kuzungumza na watendaji wa mahakama hiyo, ambapo kwa siku hiyo atahitimisha ziarake ya siku nne kisiwani Pemba.

No comments:

Post a Comment