HATARI KUBWA: JENGO HILI DAR KUPOROMOKA MUDA WOWOTE – VIDEO - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 17 April 2018

HATARI KUBWA: JENGO HILI DAR KUPOROMOKA MUDA WOWOTE – VIDEO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema serikali inafanya uchunguzi kuhusu mkandarasi aliyejenga jengo la ghorofa kumi lililopo Upanga ambalo nguzo zake zimepinda na kuweka nyufa, hali inayotia hofu kuwa huenda likaanguka muda wowote.

Makonda aliyasema hayo baada ya kufika katika ghorofa hilo na kushuhudia hali halisi, ambapo hatua ya awali aliyoichukua ni kuwaondoa watu wote wanaoishi ndani ya nyumba hiyo na kuwataka majirani wanaozungukwa na ghorofa hilo kuwa makini.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema ambaye naye alifika eneo la tukio na kushuhudia jengo hilo, amesema mkandarasi aliyehusika kujenga jengo hilo yupo hivyo wanamsubiri pamoja na mainjinia wa manispaa, kisha waangalie kibali kilichotolewa cha ujenzi wa ghorofa hilo ndiyo kilichotumika au la.

Aidha DC Mjema, amesisitiza majirani walio karibu zaidi na ghorofa hilo kutolala ndani kwa siku ya leo mpaka pale watakapowatangazia ili kuweza kunusuru maisha yao.

No comments:

Post a Comment