Haji Manara Atoa Kali Amkaribisha Msemaji wa Yanga Mjini "Njoo Nikupe Elimu Hii" - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 30 April 2018

Haji Manara Atoa Kali Amkaribisha Msemaji wa Yanga Mjini "Njoo Nikupe Elimu Hii"

Haji Manara Atoa Kali Amkaribisha Msemaji wa Yanga Mjini "Njoo Nikupe Elimu Hii"
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara amemkaribisha mjini Msemaji wa  Klabu ya  Young Africans, (Yanga)  Dismas Ten  kwa kumwambia anamkaribisha kumpatia elimu juu ya kazi anayoifanya.


Manara  ametoa kauli hiyo ya kumkaribiisha mjini Msemaji huyo wa Yanga baada ya Klabu yake kuifunga Yanga siku ya jana ambapo amesema alimuweka kiporo siku nyingi na kwamba alikuwa akisubiri siku ya kumpa majibu kutoka na kile achokiita mafumbo kutoka kwa Ten.

"Bro wewe bado sana..unatumia lugha za mafumbo ambazo haziisaidii klabu..huna hamasa na hutoi taarifa kiweledi na kwa matakwa ya sasa ya soka na soko..njoo nikupe elimu hii" Manara.Ameongeza "Jumatatu iliopita ulisema Yanga lazma watashinda..haya kiko wapi? leo nimeweka picha yako na nakutag ili walau watu wakujue kidogo....Hii ndio Simba bro...okey karibu town".

No comments:

Post a Comment