Daimond Alikologa Basata Nao Wamwita .... Aripoti na Mameneja Wake - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 18 April 2018

Daimond Alikologa Basata Nao Wamwita .... Aripoti na Mameneja Wake

Daimond Alikologa Basata Nao Wamwita .... Aripoti na Mameneja Wake
Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz leo, April 18, 2018 amefika ofisi za Baraza la Sanaa Taifa (BASATA).

Muimbaji huyo wa ngoma ‘African Beaut’ amefika ofisi za Basata akiongoza na mameneja wake, Sallam SK, Mkubwa Fella pamoja na msanii Harmonize.

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa Diamond ameitwa na Baraza hilo kwa lengo la kukumbushwa masuala mbalimbali kuhusiana na muziki wake.

Wiki tatu zilizopita March 23, 2018 Diamond pamoja na meneja wake walifika Basata hata hivyo pande zote mbili hazikuweka wazi kile kilichojadiliwa baina yao. Hata hivyo safari hiyo ilijiri katika kipindi ambacho nyimbo mbili za Diamond ‘Waka na Hallelujah’ zilipofungiwa. 

No comments:

Post a Comment