Conte apanga mikakati madhubuti kuikabili Southampton michuano ya FA - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 20 April 2018

Conte apanga mikakati madhubuti kuikabili Southampton michuano ya FA


Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte amesema kuwa lazima kikosi chake kiwe na mipango madhubuti katika kuhakikisha kinafanya vema kwenye mchezo wake wa nusu fainali ya michuano ya FA pale itakapo ikabili timu ya Southampton siku ya Jumapili.

Conte ameyasema hayo wakati kikosi hicho cha The Blues kikiwa katika nafasi nzuri ya kuingia nafasi ya nne ‘top four’ kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza kwakuwa na pointi 63, baada ya hapo jana kufanikiwa kuifunga Burnley mabao 2-1 ugenini na kuipa ushindani Tottenham iliyopo kwenye nafasi hiyo ya nne kwa tofauti ya alama tano.
Meneja huyo raia wa Italia amesema kuwa kamwe hatowasikiliza wale wote wanaodhani Chelsea imeshakata tamaa kwenye michuano ya FA.
Ukiachia mbali michuano hiyo ya FA, Chelsea inakabiliwa na kibarua kizito dhidi ya Swansea Aprili 28 mchezo wa ligi kuu ya Uingereza.

No comments:

Post a Comment