Comey amponda Trump, adai hana sifa ya kuwa rais - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 16 April 2018

Comey amponda Trump, adai hana sifa ya kuwa rais


Aliyekuwa mkuu wa shirika la upelelezi nchini Marekani FBI, James Comey amesema kuwa rais, Donald Trump hana maadili ya uongozi ya kuendelea kushikilia wadhifa huo.
Ameyasema hayo wakati akifanya mazungumzo na shirika la habari la ABC, ambapo amesema kuwa Trump anatabia ya kuzusha uongo mara kwa mara.
“Siamini madai yaliyopo kuhusu Trump kwamba ana matatizo ya kiakili au aliwahi kuugua ugonjwa wa kusahau, nadhani tatizo linalomsumbua ni maadili, hana maadili  ya kuwa rais, lazima aheshimu na afuate maadili ambayo ndio mzizi wa nchi hii,”amesema Comey
Hata hivyo, Saa chache baada ya kumalizika kwa mahojiano hayo, rais Donald Trump alijitokeza na kumjibu Comey akisema kuwa yeye si muongo.

No comments:

Post a Comment