CANNAVARO: TUTAPAMBANA KUUTETEA UBINGWA, NAIHESHIMU SIMBA - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 21 April 2018

CANNAVARO: TUTAPAMBANA KUUTETEA UBINGWA, NAIHESHIMU SIMBA
Nahodha wa klabu ya Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro, amesema bado wana matumaini ya kuutetea ubingwa endapo watapambana katika michezo iliyosalia.

Cannavaro ameeleza kauli hiyo mapema baada ya kuwasili nchini kutokea Ethiopia ambako walienda kushiriki mchezo wa Kombe la Shirikisho Africa dhidi ya Wolaita Dicha SC.

Nahodha huyo anaamini kwa mechi zilizosalia bado ligi ipo na wazi na watafanya juhudi za kutetea taji ili waweke rekodi ya kulitwaa mara nne mfululizo.

Mbali na kusema hivyo, Cannavaro pia amesema anawaheshimu Simba kwa kueleza kuwa ni timu nzuri na wanafanya vizuri kwa sasa pia anawaheshimu, hivyo watazidi kupigana zaidi kupata matokeo.

Yanga inaanza maandalizi leo ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Mbeya City utakaopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya.

No comments:

Post a Comment