BREAKING NEWS:DR.SHEIN AFANYA UTEUZI - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 21 April 2018

BREAKING NEWS:DR.SHEIN AFANYA UTEUZI


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanyac uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:-

OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS
1. Bwana Makame Khatib Makame ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

WIZARA YA VIJANA, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO
1. Bwana Shamuni Hashim Ali ameteuliwa kuwa Kamishna wa Idara ya Utamaduni na Sanaa katika Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

2. Bibi Fatma Hamad Rajab ameteuliwa kuwa Ofisa Mdhamini katika Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo – Pemba.

WIZARA YA HABARI, UTALII NA MAMBO YA KALE
1. Bibi Fatma Abdulrahman Khatib Babu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi katika Wizara ya Habari, Utalii, na Mambo ya Kale.

2. Bwana Ali Jaku Ali ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utalii katika Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale.WIZARA YA BIASHARA NA VIWANDA

1. Bwana Mohammed Jaffar Jumanne ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Sekretarieti ya Tume ya Ushindani Halali wa Biashara katika Wizara ya Biashara na Viwanda.

2. Bwana Kassim Seif Ali ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi katika Wizara ya Biashara na Viwanda.

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
1. Bwana Abdulrahman Mwinyi Jumbe ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Serikali.

Uteuzi huo umeanza tarehe 20 Aprili, 2018.

No comments:

Post a Comment