BAMMATA WAMETAKIWA KUTUMIA WELEDI KATIKA UONGOZI WA MICHEZO - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 19 April 2018

BAMMATA WAMETAKIWA KUTUMIA WELEDI KATIKA UONGOZI WA MICHEZO

Image result for BAMMATA
Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Baraza la Michezo la Majeshi ya Tanzania – BAMMATA wametakiwa kutumia weledi katika uongozi wa michezo ili kuhakikisha wanasimamia shughuli za maendeleo ya michezo katika vyombo vya ulinzi na usalama bila ya kuathiri sheria na kanuni za michezo husika.
Akifungua kikao cha Kamati hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya uhamiaji Zanzibar Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud alisema kufanya hivyo kutathibitisha ubora wa vyombo hivyo katika medani ya michezo na ulinzi wa nchi.
Alisema uwepo wa baraza hilo kunaongeza nafasi ya majeshi na Idara maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa na mashirikiano ya pamoja katika utekelezaji wa majukumu yao jambo ambalo litakuzwa iwapo kanuni za michezo inayoshirikishwa katika michezo ya majeshi zitazingatiwa na kuheshimiwa.

“Ni vyema katika kikao chenu muweze kujipa nafasi ya kujadili kwa kina maendeleo ya michezo na matatizo yao, kubuni mbinu za kuwasaidia wanamichezo wetu kwa lengo la kuwaendeleza kwani mnao wajibu wa kuhakikisha wanamichezo wetu wanakuwa na ratiba nzuri ya mazoezi baada ya michezo ya kila mwajka”, alisema RC Mahmoud.
Alilitaka baraza hilo kuwaendeleza waamuzi wa michezo mbali mbali wanaotoka katika vyombo vya ulinzi na usalama nchini ili waweze kufikia wiwango vya juu kitaifa na kimataifa kwa lengo la kukuza nidhamu na viwango vya ubora wa michezo nchini.
“Wanamichezo wanaotokana na vyombo hivi wakiwemo waamuzi huwa na aina Fulani ya nidhamu inayotokana na majukumu yao ya msingi hivyo wana nafasi nzuri ya kuendelea na kujiendeleza ikiwa katika uchezaji au uamuzi jambo ambalo bammata mnapaswa kulizingatia sio kwa maendeleo katika majeshi tu bali pia kwa nchi yetu”, alisisitiza Mku huyo wa Mkao.
Aidha alilishauri baraza hilo kufanya kazi kwa karibu na kamisheni ya michezo na utamaduni ya wizara ya elimu na mafunzo ya alami ili iweze kuviendeleza na kuvilea vipaji vya wanafunzi watakaoibuliwa kupitia mpango wa ‘sports 55’ ulianzishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kama njia mojawapo ya kuunga mkono juhudi zake za kuhuisha vuguvugu la michezo Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufunguliwa kwa kikao hicho, Katibu Mkuu wa BAMMATA Kanal Richard Mwandike alisema kikao hicho kina lengo la kutahmini na kupanga mikakati ya kufanuikisha mashindano ya majeshi itakayofanyika baadae mwaka huu.

“Tumekuwa na kawaida ya kukutana kabla n ahata baada ya michezo yetu ili kuweza kufanya tathmini na kunga mipango ya michuano ijayo ambayo itakuwa na michezo miwili zaidi kutoka 7 hadi 9 iliyofanyika mara ya mwisho ili kutoa nafasi kwa wananmichezo wengi zaidi waweze kushiriki na kuonesha vipaji vyao”, alisema Kanal Mwandike
Baraza hilo linakutana chini ya uongozi wa Makamo Mwenyekiti wake Naibu Kamishna Gidion Nkana na wajumbe kutoka vikosi mbali mbali vya ulinzi na usalama pamoja na Idara maalum za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambapo pamoja na mambo mengine litaamua tarehe za mashindano ya majeshi nchini ambayo hutumika kupata timu za taifa za majeshi zitakazoenda kushindana katika mashindano mbali mbali ya kimataifa kiwemo ya majeshi ya Afrika Mashariki

NA MZEE GEORGE.

No comments:

Post a Comment