Baba amrusha mwanaye wa mwaka mmoja kutoka juu ya paa - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 16 April 2018

Baba amrusha mwanaye wa mwaka mmoja kutoka juu ya paa

Mwanaume mmoja kutoka nchini Afrika Kusini ameingia kwenye headlines za vyombo vya habari duniani kwa kitendo alichokifanya cha kushangaza baada ya kumtupa mtoto wake kutoka juu ya bati la nyumba yake.

Inaelezwa kuwa mwanaume huyo ambaye ana umri wa miaka 38 nyumba yake ilitakiwa kubomolewa na polisi kutokana na kuishi katika makazi ‘haramu’ na katika kufanyika kwa zoezi hilo aliamua kupinga nyumba yake kubomolewa kwa kutishia kumtupa mtoto wake.

Mwanaume huyo alipanda juu ya nyumba yake akiwa amemshikilia mtoto wake huyo wa kike wa mwaka mmoja na pindi askari alipomsogelea alimwachia mtoto huyo na bahati nzuri alidakwa na moja ya maaskari waliokuwa eneo hilo.

Mtoto huyo anaripotiwa kutojeruhiwa na mwanaume huyo amekamatwa na kufunguliwa kesi ya jaribia la kuua.


No comments:

Post a Comment