AKUTWA LIVE CHUMBANI NA MUME WA MTU, KANGA MOJA - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 19 April 2018

AKUTWA LIVE CHUMBANI NA MUME WA MTU, KANGA MOJA

Mwenye mume akionyesha picha ya ndoa.

Amenaswa! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mwanamke mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja kukutwa chumbani kwa mume wa mtu na mke wa Ramadhan Mikaka, Tatu Khamis maeneo ya Kibaha Kwa Mathias mkoani Pwani.

NI JUMAPILI ILIYOPITA
Tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita ambapo imeelezwa kuwa, Tatu alikwenda kwa wazazi wake baada ya kutokea hali ya kutoelewana na mumewe na aliporudi siku ya tatu, ndipo akakuta chumbani kwake kuna ‘kifaa kipya’ kikiwa na upande wa kanga huku mumewe akiwa ametinga pensi.

TUJIUNGE NA CHANZO
Mnyetishaji wetu alieleza kuwa, awali wanandoa hao walikuwa wakiishi kwa raha mustarehe lakini ghafla mdudu nuksi aliingia kwenye ndoa yao iliyodumu kwa takriban miaka kumi na ushee.

ATIMKIA KWA MAMA’KE
Mnyetishaji wetu alizidi kudai kuwa, mdudu nuksi aliendelea kuishambulia ndoa hiyo hali iliyosababisha Tatu afungashe virago na kurudi kwa wazazi wake, maeneo ya Kibaha Msikitini.
“Akiwa kwa wazazi wake machale yalimcheza na kuamua kurudi kwa mumewe usiku mzito huku kimvua kilichoambatana na ubaridi kikinyesha ambapo aliambatana na mama yake aitwaye Asha Kimaro pamoja na jirani mmoja ili wakayamalize usiku ili akalale kwa mumewe,” alidai mnyetishaji wetu.
Siku ya ndoa yao.

AKUTA KIFAA KIPYA LIVE
Mnyetishaji huyo alizidi kutiririka kuwa, Tatu akiwa na ujumbe huo walikwenda kwenye nyumba aliyokuwa akiishi na mumewe ambapo walipofika mke akagonga hodi, mumewe akaanza kumuuliza kuwa yeye ni nani?
“Tatu baada ya kujitambulisha mume alianza kumuuliza maswali akiwa ndani bila kufungua mlango lakini mabishano yalipozidi, mumewe alifungua mlango ndipo timbwili lilipozuka baada ya Tatu kukuta kuna kifaa kipya ndani,” alisema mnyetishaji huyo.

WAAMBULIA MAUMIVU
Kwenye timbwili hilo, Tatu na mama yake walijikuta wakishambuliwa na mumewe pamoja na mwanamke huyo ambapo Tatu alipata maumivu kichwani huku mama yake akivunjika kidole.


WAKITINGA POLISI
Kufuatia sakata hilo, siku iliyofuata (Jumatatu), Tatu alikimbilia Kituo Kidogo cha Polisi cha Mkuza na kuwafungulia shitaka la shambulio mumewe na mwanamke aliyemkuta ndani ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja kwenye jalada lenye namba MKZ/ RB/253/2018.

POLISI WAZINGIRA NYUMBA
Kufuatia kesi, polisi walifika na kuizingira nyumba ya mwanaume huyo lakini walimkuta mwanamke huyo mpya peke yake ambapo walimkamata na kumpeleka Kituo cha Polisi cha Wilaya ya kibaha kwa mahojiano zaidi.

MWANAUME NAYE ADAKWA 
Mwanahabari wetu juzi Jumanne alimpigia simu mwanaume huyo ili aweke wazi kilichojili kwenye sakata hilo ambapo simu yake haikuwa hewani, baadaye Amani likanyetishiwa kuwa mwanaume huyo naye alikamatwa na kuswekwa lupango wakati alipokuwa kwenye harakati za kumnasua mwanamke aliyekutwa naye chumbani.
Mtuhumiwa baada ya kunaswa na polisi.


TUMSIKILIZE TATU SASA
Mwanahabari wetu alizungumza na Tatu kuhusiana na tukio hilo ambapo alisema; “Ramadhani ni mume wangu wa ndoa ambaye nimeishi naye kwa zaidi ya miaka kumi, mwanzo ndoa yetu ilikuwa raha mustarehe lakini ghafla ikaanza mizozo ya hapa na pale hali iliyonifanya nirudi kwa wazazi wangu ili wamuite na kutusuluhisha.

“Nilikaa kwa wazazi wangu siku tatu lakini ghafla mida ya saa tatu usiku machale yakanicheza ingawa mvua ilikuwa ikinyesha lakini nikaamua kuwaambia mama na jirani yake mmoja mtu mzima wanisindikize kwa mume wangu wakatusuluhishe ili ikiwezekana nikalale huo.

Safari ya kuelekea kituo cha polisi.

“Lakini tulipofika kwa mume wangu nilianza kugonga mlango huku nikimuita kwa sauti nikashangaa mwenzangu hataki kunifungulia ambapo tulianza kujibizana yeye akiwa ndani. “Alipoona nimekazania kumtaka anifungulie aliamua kufungua mlango kwa hasira ambapo nami nilijaribu kuingia kinguvu, lahaulaaa… ile kuingia tu nikamkuta laivu yuko na mwanamke ambapo katika purukushani walianza kunichangia na kunishambulia ambapo mama alipotaka kunigombelezea naye aliumizwa kidole cha kati mkono wa kushoto.

“Yule jirani alipoona vurugu imezidi alitafuta upenyo na kukimbia, mimi nilipoona mambo mazito niliamua kukimbilia polisi ili kujiokoa, nikachukua RB na leo tumekuja kuwachukua na polisi, tumemkuta mwanamke tu, mume wangu hakuwepo.”
Gazeti hili linaendelea kufuatilia kwa karibu sakata hilo na kitakachojiri tutakiandika kupitia magazeti ya Global Publishers.
 Stori: Richard Bukos na Erick Evarist, Amani

No comments:

Post a Comment