Wednesday, 19 September 2018

KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA COASTAL UNION, KINDOKI KAMA KAWA


Kikosi cha Yanga kitakachoanza dhidi ya Coastal Union leo, mechi ya Ligi Kuu Bara

1. Klaus Kindoki
2. Paul Godfrey
3. Gadiel Michael
4. Andrew Vincent 
5. Kelvin Yondani
6. Pappy Kabamba
7. Mrisho Ngassa
8. Feisal Salum 
9. Heritier Makambo
10. Ibrahim Ajibu
11. Deusi Kaseke

Kikosi cha akiba

12. Beno Kakolanya
13. Abdallah Shaibu 
14. Jaffary Mohammed
15. Thaban Kamusoko
16. Raphael Daudi
17. Matheo Anthony 
18. Amis Tambwe

KUMBE ZAHERA MJANJA!! HUU NDIYO MKENGE ALIOWAINGIZA COASTAL UNION


Kocha Mkuu wa Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera amewaambia mabeki wa timu pinzani kuwa yeye hana hofu wao waendelee kumkaba mshambuliaji wake Heritier Makambo kwani wapo Ibrahim Ajibu na Mrisho Ngassa wenye uwezo mkubwa wa kufunga.

Kauli hiyo aliitoa baada ya mechi ya Ligi Kuu Bara kumalizika kwa Yanga kuwafunga Stand United mabao 4-3 mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mechi hiyo, mabao ya Yanga yalifungwa na Andrew Vincent ‘Dante’, Deus Kaseke, Ngassa na Ajibu huku mabao matatu ya Stand yakifungwa na Alex Kitenge.

Zahera alisema anafahamu hivi sasa mshambuliaji wake Makambo anapaniwa na kila timu inayokutana naye kutokana na kutajwa kwenye vyombo vya habari na kusababisha kuzua hofu.

Zahera alisema, alichokifanya hivi sasa ni kutengeneza washambuliaji wengine watakaofanya kazi ya Makambo ambayo ni kufunga mabao katika kila mechi baada ya kuona mshambuliaji huyo kapaniwa na mabeki wa timu pinzani.

Aliongeza kuwa, amefurahishwa na jinsi washambuliaji wake wengine Ajibu, Ngassa na Kaseke anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji, kufuata maelekezo yake aliyowapa kwa kufanyia kazi na kupata ushindi huo wa mabao 4-3.

“Lipo wazi kabisa, kila timu tunayokutana nayo hivi sasa inamuangalia Makambo pekee, wenyewe wanaamini wakimzuia huyo ndiyo basi Yanga hatuwezi kupata ushindi, kitu ambacho siyo.

“Hivyo, niwaambie kuwa, wao waendelee kumkaba Makambo na wawaache wachezaji wengine waendelee kufunga mabao, ninaamini kwa wachezaji hawa nilionao nina uhakika wa kupata matokeo mazuri katika kila mechi.

“Nimefurahishwa na safu yangu ya ulinzi inayocheza kwa kujiamini na kutengenezeana nafasi za kufunga kama ilivyokuwa mchezo wa ligi na Stand ambao wachezaji wangu walitumia vema kila nafasi waliyokuwa wanaipata.

 “Naamini mimi nina wachezaji wengi ambao wanaweza kufunga mabao, ukimzuia Ajibu atafunga Makambo, ukimzuia Makambo atafunga Ajibu, hivyo sina shida,” alisema Zahera.

Monday, 17 September 2018

DK.SHEIN AKUATANA NA BALOZI WA KENYA.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)  akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Kenya Nchini Tanzania Mhe.Dan Kazungu alipofika kujitambulisha leo Ikulu Mjini Zanzibar akifuatana na ujumbe wake,[Picha na Ikulu.] 17/09/2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na  Balozi wa Jamhuri ya Kenya Nchini Tanzania Mhe.Dan Kazungu alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kujitambilisha akiwa  na ujumbe wake (hawapo pichani),[Picha na Ikulu.] 17/09/2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiagana na  Balozi wa Jamhuri ya Kenya Nchini Tanzania Mhe.Dan Kazungu baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kujitambulisha,[Picha na Ikulu.] 17/09/2018. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na  Balozi wa Jamhuri ya Kenya Nchini Tanzania Mhe.Dan Kazungu baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo alipofika kujitambulisha akifuatana na ujumbe wake (hawapo pichani),[Picha na Ikulu.] 17/09/2018.

Na Ramadhan Othman Abdalla

Breaking: Mtangazaji wa Clouds Fm Soudybrown na msanii Maua sama wamekamatwa na Polisi (VIDEO)

Mtangazaji wa Clouds Fm Soudy Brown wa Shilawadu pamoja na muimbaji wa muziki, Maua Sama wanadaiwa kushikiliwa na Jeshi la polisi Dar es salaam.
Wawili hao wanadaiwa kukamatwa na Polisi Kinondoni lakini jioni hii tayari wameshahamishiwa Central Polisi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha uhakika, kimedai wawili hao walishikwa siku ya jana baada ya kupost video mtandaoni inayowaonekana watu wakicheza wimbo ‘Iokote’ wa Maua Sama huku wakiwa wanakanyaga hela.
Bongo5 tumenasa video inayowaonyesha baadhi ya wafanyakazi Clouds Media wakiingia Polisi Central.
Kwa taarifa zaidi endelea kukaa na Bongo5.

By Ally Juma

BREAKING: MEDDIE KAGERE MWANASOKA BORA LIGI KUU BARA


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza rasmi straika wa klabu ya Simba, Meddie Kagere kuwa mchezaji bora wa mwezi Agosti katika Ligi Kuu Bara.

Kagere amekuwa mchezaji wa kwanza katika msimu huu wa 2018/19 kushinda tuzo hiyo ambayo hutolewa kila baada ya mwezi mmoja.

Straika huyo ameisaidia Simba kuibuka na alama 6 za Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya City huku akifunga mabao matatu.